Home Simba SC PERFECT CHIKWENDE WA SIMBA ATAJA TUZO ANAYOITAKA BONGO

PERFECT CHIKWENDE WA SIMBA ATAJA TUZO ANAYOITAKA BONGO


KIUNGO mshambuliaji wa Simba raia wa 
Zimbabwe, Perfect Chikwende, amesema kwa sasa anapambana juu chini kabla ya msimu kwenda ukingoni awe tayari ameweka tuzo moja kwenye kabati lake.

Chikwende anaitaka Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Mashabiki, ambayo imeanza kutolewa na klabu hiyo miezi miwili iliyopita.

Mpaka sasa, tuzo hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Emirates Aluminium Profile, imechukuliwa na Luis Miquissone raia wa Msumbiji na Mkenya, Joash Onyango.

Onyango alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Machi, huku Luis akichukua tuzo hiyo mwezi Februari akiwa ndiye amefungua dimba.

Akizungumza na Spoti Xtra, Chikwende alisema: “Natamani na mimi nichukue tuzo ya mwezi kama wenzangu kwa sababu ni kitu ambacho kila mchezaji anakitamani, nitaongeza juhudi na kupambana zaidi ili niipate kabla ya msimu kuisha.”



SOMA NA HII  USAJILI SIMBA WAMSONONESHA TUNDA MAN....ADAI YUKO TAYARI KUTEMBEZA BAKULI LA KUPATA PESA ZA USAJILI...