MABOSI wa Yanga leo Aprili 20 wameamua jambo lao ambapo watamtangaza mrithi wa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alichimbishwa kazi Machi 7 kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo.
Baada ya mchujo wa muda mrefu hatimaye Mtunisia Nasreddine Nabi anatarajiwa kutambulishwa leo baada ya kutua Bongo majira ya saa 7:30 mchana.
Kocha huyo leo atapata nafasi ya kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Gwambina ambao utachezwa Uwanja wa Mkapa.
Yanga kwa sasa ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi ambaye ameiongoza timu hiyo kwenye mechi mbili ilikuwa Yanga 1-1 KMC na Yanga 1-0 Biashara United.
Kocha huyo aliwahi kuinoa Klabu ya Al Merrikh ya Sudan ambayo iliwah kufundishwa pia na Kocha Mkuu, Dider Gomes, raia wa Ufaransa ambaye kwa sasa anaiona Simba.
Anapewa nafasi ya kukaa kwenye benchi pale ambapo Yanga itamenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa, Mei 8.