IMEELEZWA kuwa Mwinyi Zahera aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga tayari ameanza kazi ndani ya Simba akiwa katika idara ya kusaka vipaji na anatarajiwa kutambulishwa rasmi kwa mashabiki.
Inakuwa ni mara ya pili kwa Zahera kutajwa kuibuka ndani ya Simba ambapo awali ilielezwa kuwa atakuwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi.
Mmoja wa watu wa ndani kutoka Simba ameliambia Spoti Xtra kuwa Zahera ameanza kazi kwa muda wa miezi mitatu huku uwepo wake ukiwa ni wa siri.
“Ni kweli hilo suala la Zahera kuwa mkuu wa masuala ya kusaka vipaji ingawa imekuwa kwa siri kwa kuwa uongozi wenyewe hautaki presha kutoka kwa mashabiki kutokana na hali ilivyo ndani ya timu,” ilieleza taarifa hiyo.
Simba ipo chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa akishirikiana na Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi.