Home Yanga SC SARPONG APITISHA SIKU 136 BILA KUFUNGA YANGA

SARPONG APITISHA SIKU 136 BILA KUFUNGA YANGA

 


MICHAEL Sarpong, mshambuliaji wa kikosi cha Yanga raia wa Ghana ametimiza siku 136 ambazo ni sawa na saa 3,264 za kucheza bila kufunga bao kwenye mechi zote za ushindani ikiwa ni zile za Ligi Kuu Bara na Shirikisho.

Kwenye ligi Yanga ina pointi 57 baada ya kucheza mechi 26 na ina mabao 41 amehusika kwenye mabao 7, alifunga mabao manne, pasi mbili za mabao na alisababisha penalti moja kwenye mchezo dhidi ya KMC, Uwanja wa CCM Kirumba.

Ukurasa wa mabao alifungua Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Yanga 1-1 Tanzania Prisons, ilikuwa ni Septemba 6 kisha Oktoba 31 akawatungua Biashara United, Uwanja wa Karume. Novemba 7 akawatungua Simba ilikuwa ni kwa mkwaju wa penalti na Desemba 6 alifunga akaunti yake ya mabao kwa kuwafunga Ruvu Shooting ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Nyota huyo hivi karibuni alisema kuwa anatambua kwamba mashabiki wanahitaji kumuona akifunga jambo ambalo anapenda kuona likitokea.

Wakati ubao ukisoma Yanga 3-1 Gwambina, Uwanja wa Mkapa alimpa pasi mshikaji wake Said Ntibanzokiza.

SOMA NA HII  YANGA WAIBUKA NA 'MIHOGO PARTY'....ALLY KAMWE AFUNGUKA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI...