Home Yanga SC MTUNISSIA WA YANGA AKAA KIKAO NA WACHEZAJI,

MTUNISSIA WA YANGA AKAA KIKAO NA WACHEZAJI,


 NASREDDINE Nabi, mrithi wa mikoba ya Cedrick Kaze ndani ya kikosi cha Yanga ameanza kazi na kikao kizito kwa wachezaji wa timu hiyo mara baada ya kutambulishwa kuwa kwenye benchi la ufundi.


Kocha huyo kesho anatarajiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mara ya kwanza ikiwa vibali vyake vitakamilika kwa kuwa mpaka jana walikuwa ilikuwa kwenye hatua za mwisho kupatikana.

Habari kutoka kambini zimeeleza kuwa raia huyo wa Tunissia aliwaambia wachezaji wake kwamba ni lazima wabadili gia hasa kwenye upande wa nidhamu ili kuweza kupata matokeo kwenye mechi zao zijazo.

Habari kutoka Yanga zimeeleza:-“Kocha wa Yanga alikaa na wachezaji wote kikao kizito na alizungumza nao masuala mengi kwa msistizo mkubwa jambo la kwanza alianza kuhusu nidhamu.

“Hapo alipata muda wa kuzungumza na wachezaji wote ikiwa ni pamoja na Saido Ntibanzokiza ambaye hivi karibuni alikuwa kwenye mzozo na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzake kwa kitendo cha kuomba kufanyiwa mabadiliko.

“Pia amewaambia kwamba anahitaji kuona wanachukua  Kombe la Shirikisho ambalo lipo mbele yao kwani wametinga hatua ya 16 bora na kuhusu kombe la ligi kasema ni suala la muda.

“Migogoro ya wachezaji pamoja na viongozi amekataa na kusema kuwa wao ni kitu kimoja na lazima wapambane bila kuwa na tofauti zozote zile hiyo ni maana halisi ya timu,” ilieleza taarifa hiyo.

Nabi aliliambia Championi Jumamosi kuwa anahitaji vitendo zaidi  kwa kila mchezaji kuliko porojo kwani yeye ni mtu wa matokeo.

SOMA NA HII  MAYELE AENDELEA ALIPOISHIA ...ATIA KAMBANI GOLI TATU MWENYEWE....AZIZ KI , MAKAMBO WANOGESHA 'SHOW'....