Home Simba SC MUGALU AWA SHUJAA SIMBA IKIIRARUA DODOMA JIJI 3-1

MUGALU AWA SHUJAA SIMBA IKIIRARUA DODOMA JIJI 3-1

 


DAKIKA 90 zimemalizika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kati ya Simba na Dodoma Jiji kwa wekundu hao wa Msimbazi kushinda mabao 3-1.

Katika mchezo huo ulioanza saa 1:00 usiku katika dimba la Mkapa Simba imeonekana kulitawala vizuri eneo la kiungo.

Katika eneo hilo Simba imeanza na Luis Miqussone, Clatous Chama, Mzamiru Yassin na Rally Bwalya ambao wamefanikiwa kwa asilimia nyingi katika kuifungua Dodoma.

Awali Dodoma ilianza kwa kupishana na Simba kwa muda usiopungua dakika mbili baada ya hapo ikawa inacheza nyuma ya mstari wa kati.

Kucheza nyuma ya mstari ilikuwa kama kuiruhusu Simba ifanye inachohitaji kwani iilimikiki vyema eneo la kiungo hadi ikafanikiwa kupata bao dakika ya nane kupitia kwa mshambuliaji wake Chriss Mugalu.

Baada ya Simba kupata bao iliendelea kufanya mashambulizi kwa kasi ambayo hayakuwa na matunda yoyote.

Baada ya Simba kushambulia sana Dodoma ilifanya shambulizi moja la kushtukiza ambalo  liluzuiwa na mabeki wa Simba kwa kutolewa nje na kuwa kona.

Kona hiyo ilienda kupigwa na Abubakar Ngelema kisha Cleophas Mkandala akatumbukiza mpira wavuni dakika ya 28.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika ubao ulikuwa unasoma 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana Simba ikionekana kulisakama lango la Dodoma.

Mbali ya Simba kushambulia, Dodoma nayo ilijaribu kutoka na kufanya mashambulizi kadhaa ya kushtukiza pale ilipowapoka mpira Simba.

Baada ta mashambulizi kadhaa Simba ilijiandikia bao la pili kupitia kwa Miquissone dakika ya 55 aliyepokea pasi kutoka kwa Chama.

Simba iliendelea kuinyanyasa Dodoma na dakika ya 67 ikaandika bao la tatu kupitia kwa Mugalu ambaye pia alipokea pasi ya Chama.

Licha ya mashambulizi ya kupokezana kwa timu zote mbili, dakika 90 za mtanange huo zilimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWATUNGUA WABOTSWANA...LWANGA ATOA NENO KWA MASHABIKI WA SIMBA