Yanga SC

YANGA YAWASILI SALAMA MBEYA

admin April 27, 2021 2:48 pm

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Nassreddine Nabi leo Aprili 27 kimewasili salama Mbeya.

Safari hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wao Tanzania Prisons kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho,  hatua ya 16 bora.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 30, Uwanja wa Nelson Mandela saa 10:00 jioni.

Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold, Uwanja wa Uhuru.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wapo imara na wanaamini kwamba watafanya vizuri.

Hesabu kubwa kwa sasa kwa Yanga ni kulitwaa taji hilo ambalo lipo mikononi mwa Simba. 



MTIBWA SUGAR NA KAGERA SUGAR MAMBO MAGUMU NDANI YA LIGI LUIS, WAWA WAREJEA KIKOSI CHA SIMBA TAYARI KUIVAA DODOMA JIJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply