BADRU Mohammed, Kocha Mkuu wa Gwambina FC amesema kuwa hesabu kubwa za timu hiyo kwa sasa ni kuweza kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/21.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 30 baada ya kucheza jumla ya mechi 27.
Haijawa kwenye mwendo mzuri licha ya kwamba ana tuzo ya kocha bora wa mwezi Machi kwani katika mechi zake nne za hivi karibuni ameambulia kichapo mfululizo.
Waliacha pointi tatu mbele ya KMC, Yanga, Simba na ilipoteza pia kwa kufungwa na Mwadui ambayo inapambana kusaka nafasi ya kujinasua kutoka nafasi ya 18 ambayo imedumu nayo kwa muda mrefu.
Badru amesema:”Malengo yetu makubwa kwa sasa ni kuona kwamba timu inabaki kwenye ligi msimu ujao, matokeo ambayo tunayapata ni mabaya ila kuna kitu ambacho tunakionyesha.
“Wachezaji wamekuwa wakifanya makosa ambayo tunayafanyia kazi hivyo nina amini kwamba wale ambao wanaona wanajua kwamba Gwambina ni hodari,” amesema.