Home Yanga SC KAZI INAENDELEA, MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA KAZE UMEFIKIA HAPA

KAZI INAENDELEA, MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA KAZE UMEFIKIA HAPA


IMEELEZWA kuwa mchakato wa kumpata kocha mpya ndani ya Yanga kwa sasa umefika hatua nzuri baada ya majina matano kupitishwa baada ya makocha hao kuwa na sifa hizo wanazohitaji. 

Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa ni pamoja na Nikola Kovazovic ambaye ni kocha wa zamani wa Klabu ya Township Rollers ya Botswana, aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya TP Mazembe, Hubert Velud na kocha wa zamani wa Harambee Stars ya Kenya, Sebastian Mingne raia wa Ufaransa.

Jina lingine ambalo limewekwa kwenye meza za mabosi wa Yanga ni Miodrag Jesic raia wa Serbia ambaye huyu anapewa chapuo kubwa la kuja Bongo.

Kocha huyo aliwahi kuifundisha Klabu ya Al Merrikh ya Sudan iliyokuwa kundi moja na Simba kwenye hatua ya makundi.

Pia timu hiyo aliwahi kufundisha Didier Gomes ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi cha Simba.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa majina hayo yanafanyiwa mchakato ili kuona ni nani ambaye atapita kuwa mrithi wa Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo.

“Kuna majina mengi ambayo yalikuwa yanahitaji kazi Yanga ila haiwezi kuwa rahisi kumchukua kocha ambaye hana uzoefu, yapo zaidi ya majina matano ambayo yanatazamwa kwa ukaribu na muda wowote kuanzia sasa kocha atatangazwa,” ilieleza taarifa hiyo.


Kwa sasa Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 51 ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi ambaye leo ana kibarua cha kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United.

SOMA NA HII  ZA NDAANI KABISAAA...YANGA WALIIZIDI SIMBA HAPA KWA JOB....LA SIVYO ANGEKUWA MSIMBAZI ...