Home Simba SC FRAGA – MUDA WA KURUDI UWANJANI UMEKARIBIA

FRAGA – MUDA WA KURUDI UWANJANI UMEKARIBIA


KIUNGO Gerson Fraga amewapa habari njema mashabiki wa Simba kuwa amepona majeraha yake ya muda mrefu na muda sio mrefu atarejea uwanjani na anatamani kurudi ndani ya timu hiyo.

Fraga aliachwa na Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo kutokana na majeraha ya goti aliyopata katika mchezo dhidi ya Biashara United ambayo yalifanya afanyiwe upasuaji ambao umemfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa za taifa za vijana za Brazil, baada ya kuuguza majeraha yake kwa takribani miezi saba, amewahakikishia mashabiki wa Simba kuwa yuko fiti na yuko tayari kurudi kwenye timu hiyo ambayo inatamba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivi sasa.

“Muda wa kurudi uwanjani unakaribia. Namshukuru kila mmoja kwa sapoti. Mkata umeme nitarudi haraka haraka. Nakuja,” ameandika Fraga kwenye ukurasa wake wa Instagram. Wakati Fraga akiweka wazi nia ya kurejea Simba, mmoja wa viongozi wa timu hiyo alisema itategemea na mahitaji ya benchi la ufundi chini ya kocha Didier Gomes Da Rosa.

SOMA NA HII  ANAYEFUATA KUTAMBULISHWA SIMBA HUYU HAPA....TAYARI YUKO ZAKE ZNZ MAPEMA TU...