Home Yanga SC MAENDELEO YA KISINDA NA DICKSON JOB YALETA MATUMAINI YANGA

MAENDELEO YA KISINDA NA DICKSON JOB YALETA MATUMAINI YANGA


 NYOTA wawili wa kikosi cha Yanga, ambao walipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri jambo ambalo linaleta matumaini kwa nyota hao kurejea kwenye majukumu yao.

Job ambaye ni beki ikiwa ni mchezo wake wa pili kucheza ndani ya Yanga akitokea Mtibwa Sugar alipata tatizo la maumivu ya misuli ya nyama za paja jambo lililomlazimu kuomba mabadiliko na nafasi yake kuchukuliwa na Bakari Mwamnyeto.

Mchezo wa kwanza wa Job ilikuwa Yanga 1-0 Biashara United na mchezo wa pili ambao hakuyeyusha dakika zote 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 3-1 Gwambina FC.

Mwingine ni Tuisila Kisinda ambaye alipata maumivu ya bega yeye nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Said Ntibanzokiza.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa nyota hao wanaendelea vizuri kwa sasa.

SOMA NA HII  NDOA YA MKUDE NA YANGA SHAKANI....'WENYE TIMU' WASHINIKIZA 'APIGWE PANGA' DIRISHA DOGO..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here