Home CAF MANULA :- NA BADO CAF…MPAKA KIELEWEKE..!!!

MANULA :- NA BADO CAF…MPAKA KIELEWEKE..!!!


KIPA wa Simba, Aishi Manula amesema wanatamani kusonga mbele zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kutinga hatua ya robo fainali,wakiichapa  AS Vita ya DR Congo kwa  jumla ya mabao 5-1, nyumbani na ugenini.

Manula amesema kwamba kila hatua katika mechi za Caf wanajua ugumu wake, hivyo wanaongeza umakini wa kuhakikisha wanaandika rekodi ya aina yake kwa msimu huu.

“Tumepambana na hatuwezi kujibweteka kuona tumemaliza kila kitu baada ya kufika hatua ya robo fainali, maana hiyo ni hatua ngumu, lazima tujipange kikamilifu ili tuzidi kwenda mbali zaidi ya hapa,” amesema na ameongeza kuwa;

“Ni kweli tumepambana kadri tulivyoweza hadi tulipofika, tukiungwa mkono na mashabiki ambao wamekuwa bega kwa bega na sisi kwa nyakati zote, bado tuendelee kuwaomba kwamba tuungane kwa umoja wetu ule ule ili kuona tunafika mbali zaidi ya robo fainali,”amesema.

Manula amesema nje na mechi za Caf, wanahitaji kufanya vyema Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam, ili kutetea mataji hayo baada ya kuwa mabingwa msimu ulioisha.

“Ndio maana nasema bado tuna kazi ngumu hakuna kulala, tutapambana Caf, ligi kuu na ASFC ambazo vyote tulichukua taji msimu ulioisha na sasa tunahitaji kutetea kwa msimu huu,”amesema.

SOMA NA HII  ISHU YA MABEKI WA SIMBA KURUDIA MAKOSA ITARUDISHA MABAO MATANOTANO KIMATAIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here