Home Yanga SC MITAMBO HII YA MABAO NDANI YA YANGA YAREJESHA TABASAMU

MITAMBO HII YA MABAO NDANI YA YANGA YAREJESHA TABASAMU

 


JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa uwepo wa washambuliaji wake wawili ambao ni Michael Sarpong raia wa Ghana na Yacouba Songne raia wa Burundi kwenye mazoezi unampa nguvu ya kufanya vizuri kwenye mechi zake.

Sarpong amefunga mabao manne na pasi moja ya bao huku Yacouba akitupia mabao manne na pasi nne na kuwafanya jumla wahusike kwenye mabao 13 kati ya 36 baada ya kucheza mechi 23.

Tayari wameanza mazoezi kambini Kigamboni kwenye kijiji cha Avic kujiweka sawa kabla ya kurejea kwa Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwambusi alisema kuwa wachezaji wake wameanza kuimarika jambo ambalo linampa nguvu ya kuamini kwamba watafanya vizuri.


“Kazi ambayo ipo kwa sasa ni kuweza kuona namna ambayo tunaweza kuwa imara. Nimewaona vijana ikiwa ni pamoja na Sarpong, (Michael), Yacouba, (Sogne) pamoja na wachezaji wengine ni furaha kwangu na timu kiujumla,” alisema.    

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ANATUMIA NDOTO KUPANGA KIKOSI...ALIOTA FARID ANAIFUNGA TP MAZEMBE