Home Ligi Kuu SIMBA YASHINDA 5G MBELE YA MTIBWA SUGAR KWA MKAPA

SIMBA YASHINDA 5G MBELE YA MTIBWA SUGAR KWA MKAPA

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,  Simba leo Aprili 14 wameibuka na ushindi wa.mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo, Uwanja wa Mkapa. 


Chini ya Didier Gomes Simba ilianza kwa kasi na kufanikiwa kupachika bao la Kwanza dakika ya 7 kupitia mwa Clatous Chama. 


Alikuwa ni Luis Miquissone ambaye alichezewa faulo kisha jukumu la kupiga faulo hiyo akapewa Chama aliyefunga bao hilo la kwanza akiwa nje ya 18.


Bao la pili lilipachikwa na Rary Bwalya dakika ya 19 na bao la tatu lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 43 na kuwafanya Simba kuenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa 3-0.


Kipindi cha pili Simba waliongeza mabao mawili kupitia kwa Kagere dk 51 na Luis Miquissone dakika ya 73.


Simba wanasepa jumla ya pointi nne kwa Mtibwa Sugar kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri,Morogoro ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-1 Simba

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO