Home Yanga SC YANGA WAANZA NA SAFU YA ULINZI

YANGA WAANZA NA SAFU YA ULINZI

 


JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha wa Yanga amesema kuwa ataanza kuboresha safu ya ulinzi ili isifanye makosa ya kuruhusu mabao kwenye mechi zote za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Ukuta wa Yanga unaoongozwa na nahodha, Lamine Moro pamoja na Bakari Mwamnyeto umeruhusu jumla ya mabao 15 baada ya kucheza mechi 24 na mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye sare ya kufungana mabao 3-3 unashikilia rekodi ya kuwa ni mabao mengi kwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwambusi alisema kuwa safu ya ulinzi inahitaji mabadiliko ili kuwa bora jambo ambalo linamfanya awe anabadilisha pacha itakayoanza kulinda lango.

Wakati ubao ukisoma Yanga 1-1 KMC, Uwanja wa Mkapa Mwambusi alianza na Lamine pamoja na Abdalah Shaibu, “Ninja’ kwenye upande wa mabeki wa kati.

Mwambusi alisema:”Tunajaribu kufanya mabadiliko sanasana ni kuweza kufanya marekebisho kwenye eneo la ulinzi wakati mwingine unaona tunaanza na Juma Makapu na Lamine, awali ilikuwa ni Mwamnyeto, (Bakari) na Lamine na Ninja na Lamine, na unaona kwamba haturuhusu mabao mengi .

“Tumeona makosa ambayo yanatufanya tuwe tunaruhusu mabao, tumejua kwamba ni namna ambavyo wachezaji wanajipanga hivyo bado tupo kwenye maboresho,” alisema Mwambusi.

SOMA NA HII  DAKTARI WA VIUNGO YANGA AKOMAA NA MAXI ISHU IKO HIVI