Jana baada ya kutangazwa Kocha Bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Kocha Mkuu Didier Gomez amesema tuzo hiyo ni kwa ajili ya benchi zima la ufundi si yake peke yake.
Gomez amesema siku zote wanafanya kazi kama timu na kila mmoja anatimiza majukumu yake ipasavyo, hivyo ameamua kuitoa kwa benchi nzima la ufundi.
Gomez ,ameongeza kuwa kushinda tuzo binafsi ni jambo zuri na linaongeza morali ya kazi lakini anafurahi na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wasaidizi wake.
โNafurahishwa na wasaidizi wangu, kocha msaidizi, kocha wa utimamua wa mwili, kocha wa makipa na meneja, wanafanya kazi nzuri na hii ni tuzo yetu sote,โ amesema Kocha Gomez.
Hii ni tuzo ya kwanza ya kocha bora wa mwezi wa ligi kwa Gomez tangu alipojiunga nasi Februari mwaka huu.