Ligi Kuu

KMC YAIFUATA NAMUNGO, YAPIGA HESABU POINTI TATU

admin May 7, 2021 7:47 am


UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa unazihitaji pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa, Mei 9.

Leo kikosi hicho kinatarajia kuweza kuwasili Ruangwa kukamilisha maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Huo unakuwa mchezo wa pili kwa msimu huu kwa KMC kukutana na Namungo ambapo ule wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma KMC 3-0 Namungo.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao ila wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tupo tayari na wachezaji wapo vizuri imani yetu ni kuona kwamba tunashinda mchezo wetu.

“Kila timu kwa sasa inahitaji pointi tatu hata sisi tunahitaji hivyo tutapambana mashabiki watupe sapoti,”.

MANCHESTER UNITED YATINGA FAINALI EUROPA LEAGUE VIDEO:  MECHI YA SIMBA V YANGA HAWA HAPA WAMESHIKILIA USHINDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply