Ligi Kuu

BREAKING: MCHEZO WA SIMBA V YANGA WAGHAIRISHWA

admin May 8, 2021 3:47 pm


 MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga uliotarajiwa kuchezwa leo Mei 8 umeahirishwa.

Sababu kubwa ya mchezo wa leo kuahirishwa ni kutokana na mabadiliko ya muda wa awali ambao ulipangwa kuwa saa 11:00 jioni ila ghafla Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) likatuma taarifa ya kubadili muda mpaka saa 1:00 usiku.

Kwa mujibu wa Yanga wameeleza kuwa hawawezi kucheza mchezo huo kwa kuwa TFF imekiuka kanuni ya kubadili muda  kanuni ya 15, (10) za Ligi Kuu Bara ambayo inaeeleza kuwa;”Mabadiliko yoypte ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali,”.

Yanga ilipeleka kikosi uwanjani saa 11: 00 na wachezaji walifanya warm up kisha Simba walifuata baadaye.

RASMI KIKOSI CHA SIMBA KINACHOTARAJIWA KUANZA LEO DHIDI YA YANGA, UWANJA WA MKAPA SIMBA: TUMESHANGAZWA NA KILICHOTOKEA, TULIJIAANDAA KUCHEZA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply