Ligi Kuu

WANAUME 22 LEO KAZINI KUSAKA POINTI TATU

admin May 11, 2021 6:47 am


LEO Mei 11, Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kutakuwa na mchezo mmoja kwa wanaume 22 kusaka pointi tatu muhimu.

Mwadui FC ya Shinyanga itawakaribisha ndugu zao Kagera Sugar, Uwanja wa Mwadui Complex.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi ambazo timu hizo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja.

Mwadui FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza jumla ya mechi 28 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 17 na ina pointi 27 baada ya kucheza jumla ya mechi 28.

KUMBE SOLSKAJER HAFURAHISHWI NA KAMPENI ZA NEVILE SHIRIKISHO NI MWADUI V YANGA, SIMBA V DODOMA JIJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply