WEKA kando ishu ya wachezaji 24 kukwea pipa kuelekea Afrika Kusini, usiku wa Mei 11 kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kusini dhidi ya Kaizer Chiefs unaotarajiwa kuchezwa Mei 15, unaambiwa mabegi yalikuwa gumzo jingine.
Msafara wa wachezaji ambao walikuwa ni pamoja na Aishi Manula, Ally Salim, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Chris Mugalu, Ibrahim Ame, Meddie Kagere, Mzamiru Yassin, Fracis Kahata, David Kameta.
Wengine ni Gadiel Michael, Kenedy Juma, Pascal Wawa, Clatous Chama, Taddeo Lwanga, Larry Bwalya, Hassan Dilunga, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Joash Onyango, John Bocco na Luis Miquissone.
Asilimia kubwa ya wachezaji hao walishuka na mabegi makubwa ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuwekea nguo pamoja na vibegi vingine vidogo vya mkononi jambo ambalo lilionekana kuwashangaza wasafiri wengine.
Pia viongozi ambao walikuwa kwenye msafara huo ni pamoja na Mtendaji Mkuu, Barbra Gonzalez ambaye aliingia Uwanja wa ndege majira ya saa 8:22 usiku akiwa amebeba jumla ya mabegi manne ambapo makubwa matatu na begi moja dogo.
Championi Jumatano lilipohitaji kuongea naye alisema kwa kifupi:”Kwa kweli nimechelewa ngoja nikamilishe kwanza utaratibu nitarudi,”, mpaka wanaondoka hakurudi.
Pia kwenye msafara aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Simba, Crestius Magori, Haji Manara Ofisa Habari wa Simba walikuwa ni miongoni mwa msafara huo uliowafuata wapinzani wao Kaizer Chiefs.