Home Yanga SC NYOTA YANGA HAELEWI SABABU YA BAO LA YACOUBA KUFUTWA MBELE YA NAMUNGO

NYOTA YANGA HAELEWI SABABU YA BAO LA YACOUBA KUFUTWA MBELE YA NAMUNGO


NYOTA wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Ally Mayay amesema kuwa bado hajaelewa sababu ya mwamuzi kukataa bao la Yanga ambalo lilifungwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, jana Mei 15 wakati ubao ukisoma Namungo 0-0 Yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Yacouba Songne aliweza kupachika bao dakika ya 74 lilifutwa na mwamuzi jambo ambalo lilisababisha wachezaji wakiongozwa na nahodha Bakari Mwanyeto.

Mayay ambaye ni mchambuzi wa masuala ya mpira amesema:-“Kipindi cha kwanza na cha pili ilikuwa tofauti ambapo aproach,(mbinu) ya kipindi cha kwanza Yanga walikuwa wanacheza kama ambavyo Namungo walikuwa wanacheza katikati.


“Pia hali ya uwanja ilikuwa hairuhusu kuchezea mpira kama ambavyo ingekuwa kwenye Uwanja wa Mkapa ama Uwanja wa Azam Complex.

“Kipindi cha pili kulikuwa na mabadiliko na hata speed pia ilionekana kuongezeka na vitu ambavyo vilifanya zikapatikana faulo nyingi sana.

“Hata huo uthibitisho wa goli ambalo walifunga na unaona mpaka sasa maelezo bado mpaka sasa ya sababu za huo mpira kutoenda golini haieleweki

“Kama mpira ni offside,(kuotea) kona haina offside kwa sababu kona mpira sehemu ambayo inakaa ni sehemu ya mwisho ni goal line kwa hiyo hakuna definition, (maana) ya offside hivyo sababu nyingine mwamuzi anaweza kuelezea kwa nini hakuruhusu huo mpira kuwa ni goal mpira ulioingia wavuni,” .

Ni Saido Ntibanzokiza ambaye alipiga kona hiyo na ikasindikizwa na kichwa cha nyota Tuisila Kisinda kabla ya kukutana na kichwa cha Yacouba ambaye alipachika bao hilo kwa kichwa ila lilifutwa.

SOMA NA HII  NABI :- HAWA WASAUZI MBONA MAPEMA TU....