Ligi Kuu

MTIBWA SUGAR: TUPO SEHEMU MBAYA TENA SANA

admin May 16, 2021 7:47 am


SALUM Kihimbwa nyota wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wapo sehemu mbaya sana kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara hivyo wana kazi ya kujinasua hapo walipo.

Ushindi wao wa jana mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Jamhuri kwa bao 1-0 unawafanya wafikishe jumla ya pointi 31 baada ya kucheza mechi 29.

Ni Kihimbwa mwenyewe alipachika bao hilo kwa kichwa dakika ya 5 akimalizia pasi ya George Makang’a na kuwafanya wapate pointi tatu.

Kwenye msimamo wa ligi Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 haijawa kwenye mwendo mzuri msimu huu kutokana na kupata matokeo ambayo hayawafurahishi wachezaji.

Nyota huyo amesema:”Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuipatia pointi tatu timu yangu ila tupo katika nafasi mbaya tena sana kwa sasa.

“Kikubwa kilichobaki ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu zijazo na tutapambana ili kupata matokeo chanya hivyo mashabiki watupe sapoti,” amesema.

AZAM FC: TULITUMIA NAFASI KUIFUNGA KMC, KAZI BADO NYOTA YANGA HAELEWI SABABU YA BAO LA YACOUBA KUFUTWA MBELE YA NAMUNGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply