Simba SC

KISA KAIZER… GOMES AWARUDISHA MORRISON, BOCCO NA MZAMIRU

admin May 21, 2021 9:47 am


KOCHA mkuu wa kikosi cha klabu ya Simba, Didier Gomes juzi kwenye mazoezi ya kikosi cha klabu ya hiyo kunachojiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs aliwarudisha kwenye kikosi cha kwanza nyota wa kikosi hicho, John Bocco, Mzamiru Yassin na Bernard Morrison.

Kati ya nyota hao watatu ni, John Bocco pekee ndiye aliyecheza mchezo wa kwanza Afrika kusini ambapo aliingia kuchukua nafasi ya Luis Miquissone dakika ya 84 ya mchezo, huku Morrison na Mzamiru wakishindwa kuwa sehemu ya mchezo huo.

Katika mazoezi hayo ya Jumatano, Bocco, Mzamiru pamoja na Morrison walivaa jezi za mazoezi ‘bibs’, ambazo pia zilivaliwa na wachezaji wote waliocheza mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini na kupewa program maalum dhidi ya kundi la wachezaji wengine wa akiba.

Kutokana na hali hiyo kuna uwezekano mkubwa nyota hao watatu wakawa sehemu ya mchezo wa kesho, ikiwemo kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

KAIZER CHIEF WALIVYOTUA DAR KUCHEZA NA SIMBA KESHO MWAMUZI WA SIMBA DHIDI YA KAIZER HUYU HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply