epl

LIVERPOOL YATINGA NNE BORA SASA KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA ULAYA

admin May 23, 2021 5:47 pm


WAKIWA Uwanja wa Anfield vijana wa Jurgen Klopp, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao Crystal Palace.

Ni raia wa Senegal, Sadio Mane alipachika mabo yote mawili muhimu na kuifanya timu hiyo kuushangaza ulimwengu kwa kumaliza ndani ya nne bora tofauti na awali ambapo ilianza kwa kuchechemea na kuacha ubingwa wao ukichukuliwa na Manchester City.

Sasa ni rasmi kwamba Liverpool itashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Mane kuanza kupachika bao la kwanza dakika ya 36 na 74.

Kwenye msimamo Liverpool ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 69 huku Leicester ikiwa nafasi ya tano na pointi 66 zote zimecheza mechi 38 na bingwa na anchester City mwenye pointi 86.

MORRISON: KWA SIMBA HII, MTASUBIRI MIAKA 20 HADI 30 CHELSEA YAPIGWA 2-1, YATINGA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply