FA Cup

DODOMA JIJI KAMILI GADO KUIVAA SIMBA, REKODI ZAO ACHA KABISA

admin May 25, 2021 3:47 pm


 TAYARI kikosi cha Dodoma Jiji ambao ni wapinzani wa Simba wapo ndani ya ardhi ya Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuchezwa  kesho, Uwanja wa Mkapa.

Jumla ya wachezaji 20, Benchi la ufundi pamoja na Viongozi wamewasili Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo. 


Katika mchezo huo ni mtaalamu wa kucheka na nyavu Anuary Jabir pamoja na Rajab Mgalula ambao ni majeruhi wanatarajiwa kuukosa mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa huku wachezaji wote waliobakia wakiwa katika hali nzuri kuelekea katika mchezo huo.

Dodoma Jiji imetinga hatua ya Robo Fainali ikiwa na rekodi ya kuwa timu iliyofunga mabao mengi zaidi katika michuano hiyo msimu huu, ikifunga jumla ya mabao 14 katika michezo mitatu ambayo ilikuwa Dodoma Jiji 5 – 1 Hollywood FC, Dodoma Jiji 7 – 0 Kipigwe FC na Dodoma Jiji 2 – 0 KMC.


KOMBE LA SHIRIKISHO: MWADUI 0-2 YANGA YANGA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO,

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply