Home Ligi Kuu TFF, TBLB YAINGIA MAKUBALIANO NA AZAM TV MIAKA 10

TFF, TBLB YAINGIA MAKUBALIANO NA AZAM TV MIAKA 10


 SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Azam TV Limited kwa pamoja wameingia makubaliano ya kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda wa miaka 10.

Makubaliano hayo ambayo wameingia nao yana  thamani ya Shilingi bilioni 225.6.

 Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na viongozi waalikwa waliokuwa katika hafla hiyo ya kutia saini mkataba wa Haki za Television, (Tv Rights) katika Hotel ya Hyat iliyo Posta, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema:”Nachukua fursa hii kuwapongeza Azam Media Limetide chini ya Mkurugenzi wao Tido Muhando kwa kufanikiwa kushinda tena zabuni hii hivyo kufanya kazi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania, chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuendesha ligi hii,” .

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII