Azam FC

DUBE: TUTAPAMBANA KWA AJILI YA TIMU LEO

admin May 26, 2021 5:47 am


 MSHAMBULIAJI namba moja ndani ya Azam FC, Prince Dube amesema  kuwa leo watapambana kupata ushindi mbele ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mchezo wa leo utachezwa majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni hatua ya robo fainali na mshindi wa mchezo atapambana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Dodoma Jiji ambao nao pia utachezwa leo saa 1:00, usiku Uwanja wa Mkapa.

Dube mwenye mabao 14 ndani ya ligi akiwa ni namba moja kwa utupiaji amesema kuwa wapo tayari kupata matokeo leo na watafanya kwa ajili ya timu.

“Kwa ajili ya timu yetu tutapambana ili kupata matokeo tunajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo nasi pia tutafanya hivyo.

“Kikubwa ni kwamba maandalizi yapo sawa na kila kitu kinakwenda vuzuri hatuna mashaka licha ya kwamba tunajua kwamba tutapata ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu,”.

Ni Uwanja wa Kambarage, Shinyanga mchezo huu utachezwa ili kupata mshindi ndani ya dakika 90.

HII HAPA ORODHA YA MAJEMBE YA KAZI YA NABI NDANI YA YANGA FAINALI YA EUROPA LEAGUE UNITED YAJIPA MATUMAINI KUSEPA NA KOMBE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply