Yanga SC

NABI AYATAKA MATAJI MAWILI YA SIMBA

admin May 27, 2021 6:47 am

 KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassreddine Nabi ameweka wazi kuwa wanahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na ule wa Kombe la Shirikisho.

Yanga katika Kombe la Shirikisho imetinga hatua ya nusu fainali baada ya ubao wa Uwanja wa Kambarage,Shinyanga kusoma Mwadui 0-2 Yanga 

Ndani ya Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 na kinara ni Simba mwenye pointi 61 amecheza mechi 25.

Nabi amesema:”Malengo yetu ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na ule wa Kombe la Shirikisho hilo lipo wazi na tupo tayari kwa ajili ya ushindani, “.

Bingwa mtetezi wa mataji yote hayo mawili ni Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes naye ameweka wazi kuwa anahitaji mataji hayo.

HIZI HAPA ZIMETINGA HATUA YA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO GOMES ATAJA SIRI YA SIMBA KUENDELEZA VIPIGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply