MBWANA Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa kwa kuwa ni mara yao ya kwanza kuingia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho wana mengi ya kujifunza na wanastahili pongezi.
Ameweka wazi kwamba kuondolewa kwao Mei 26 kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba katika hatua hiyo bado ni kujifunza kwa sababu wametolewa na timu bora.