kimataifa

SABABU YA CONTE KUPIGWA CHINI INTER MILAN YATAJWA

admin May 28, 2021 4:48 am


 MABINGWA wa Italia, Klabu ya Inter Milan italazimika kumlipa Antonio Conte kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni 19.8 kama fidia baada ya kusitisha mkataba.

 

Conte na Inter wamefikia makubaliano ya kusitisha mkataba baada ya kutofautiana kwenye usajili kwenye timu hiyo, anaondoka kwenye Klabu hiyo akiwa amewapa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu ya Italia (Escudetto) baada ya miaka 11.


Inter Milan walitaka kuuza wachezaji kutokana na changamoto za kiuchumi huku Conte akitaka aongezewe wachezaji ili awanie ubingwa tena wa ligi na Ligi ya Mabingwa (Uefa).


Inter Milan wamethibitisha kuachana na Conte kwa kusema:”Inter inatangaza kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha Antonio Conte, Klabu yote ingependa kumpongeza kwa kazi ya ajabu aliyoifanya, iliyohitimishwa na kubeba Scudetto, (ubingwa wa Serie A),”.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA VIDEO: DODOMA JIJI YABAINISHA KILICHOWAONDOA KOMBE LA SHIRIKISHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply