Home news AMBUNDO: WALIMU AMEKUWA AKITUSISITIZA TUFANYE KAZI KWA JUHUDI

AMBUNDO: WALIMU AMEKUWA AKITUSISITIZA TUFANYE KAZI KWA JUHUDI


 NYOTA wa kikosi cha Dodoma Jiji, Dickson Ambundo amesema kuwa mwalimu wao Mbwana Makata amekuwa akiwasisitiza kufanya kazi kwa juhudi bila kuchoka ndani ya uwanja.

Dodoma Jiji kwa msimu wa 2020/21 imekuwa na mwendo mzuri kwa timu ambazo zimepanda Ligi Kuu Bara msimu huu jambo ambalo linawapa matumaini ya kuweza kubaki kwa msimu wa 2021/22.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 39 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.

Ambundo amesema kuwa wamekuwa wakipewa maelekezo mara kwa mara na benchi la ufundi ambalo linahitaji kuwaona wakifanya vizuri.

“Mwalimu amekuwa akitusisitiza kwamba ni lazima tupambane kwa hali na mali katika kusaka matokeo kwani kazi yetu ni kuona timu inashinda.

“Ushindani ni mkubwa nasi pia tunaongeza juhudi ili kupata matokeo hakuna ambaye anapenda kuona timu ikishindwa kufanya vizuri,” amesema.

Nyota huyo aliibuka ndani ya Dodoma Jiji akitokea Klabu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo ilipata saini yake zama zile alipokuwa akitumikia Klabu ya Alliance.

SOMA NA HII  BAADA YA KUCHAPWA JUZI NA ZANACO,...MUKOKO AIBUKA NA HILI KUHUSU YANGA..AWATAJA MASHABIKI