Home Yanga SC BENCHI LA UFUNDI YANGA LAWAOMBA MASHABIKI KUSUBIRI MATOKEO CHANYA

BENCHI LA UFUNDI YANGA LAWAOMBA MASHABIKI KUSUBIRI MATOKEO CHANYA


BENCHI la ufundi la Yanga limewataka mashabiki kutulia na kusubiri matokeo chanya kwa kuwa wapo imara na watafanya vizuri katika mechi zao ambazo zimebaki.

 Hiyo ni baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara walipocheza dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

 

Timu hiyo hivi sasa ipo katika maandalizi ya mchezo wa Kombe la FA watakaocheza Jumanne ijayo dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. 


Kocha wa makipa wa timu Razack Siwa amesema kuwa kadiri ya siku zinavyokwenda anaona mabadiliko ya kikosi chake kutokana na kucheza kwa kufuata maelekezo anayowapa mazoezini.


Siwa amesema kuwa bado anaendelea kuyafanyia baadhi ya maboresho ikiwemo safu ya ushambuliaji. Aliongeza kuwa ana matumaini makubwa ya timu yake kupata matokeo mazuri sambamba na vijana wake kucheza soka safi la kuvutia kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki.

 

“Kikubwa mashabiki wanatakiwa kuwa na subira kwani bado kocha ni mpya, hivyo ana sera yake ya aina ya uchezaji.


“Hakuna kitakachoshindikana, hivi sasa tunaboresha baadhi ya nafasi ikiwemo ya ushambuliaji, hivyo mashabiki waondoe hofu wajiandae kupata furaha katika michezo ijayo ya ligi ya Kombe la FA.

 

“Mabadiliko yameanza kuonekana katika michezo iliyopita ukiwemo dhidi ya JKT Tanzania, kila shabiki ninaamini alifurahia kuona vijana wakipambana huku wakicheza soka safi la kuvutia,” amesema Siwa.

SOMA NA HII  UKWELI MCHUNGU....SAKATA LA FEI TOTO LIMEONYESHA TASWIRA HALISI YA YANGA SC...