Home news CLATOUS CHAMA ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA

CLATOUS CHAMA ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA


KIUNGO  Clatous Chama ameibuka kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Aprili ndani ya Ligi Kuu Bara.

Nyota huyo wa Simba kwa sasa amekuwa kwenye ubora ambapo ni namba moja wa kutoa pasi za mwisho akiwa  nazo 13 na ametupia mabao 7.

Amewashinda wachezaji wawili ambao ni Raphael Daud wa Ihefu FC pamoja na Prince Dube wa Azam FC.

Kwa mwezi Aprili, Chama alifunga mabao mawili na kutengeneza nafasi nne za mabao  na timu yake ilitoka nafasi ya pili mpaka nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 61.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA NA MSONGO WA KUKOSA MATOKEO MAZURI, WAISUSA SIMBA KWA MKAPA