KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa jambo lolote linaweza kutokea kwenye mpira hivyo bado wana matumaini ya kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Kaizer Chiefs.
Jana, Mei 15 Simba ilikubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa robo fainali ya kwanza Uwanja wa FNB Soccer City, Afrika Kusini.
Ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye robo fainali ya pili itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22.
Gomes amesema:”Hatujafurahia matokeo, jambo lolote linawezekana na tuna matumaini ya kupata matokeo kwa kuwa bado tuna mchezo.
“Ila ili kama tunataka kupata matokeo ni lazima tuwe bora zaidi,”.
Ikiwa Simba italazimisha sare Uwanja wa Mkapa safari yao itakuwa imeishia hatua ya robo fainali.