Habari za michezo

SAA CHACHE KABLA YA KUKUTANA NA YANGA KESHO….WASUDAN WAENDELEA KUWEWESEKA NA MAYELE…FEI TOTO KUTIWA PINGU…

admin September 16, 2022 4:16 pm


Kocha Mkuu wa Zalan, Mawein Deng amewataja Fiston Mayele na Feisal Salam ‘Feitoto’ kuwa ndio wachezaji anaowahofia zaidi hapo kesho.

Wawili hao ndio walio wafunga kwenye ushindi wa mabao 4-0 huku Mayele akiingia kambani mara 3 na Fei Toto akifunga bao moja.

Akizungumzia mchezo kwa ujumla alisema timu yake imefanyia kazi makosa waliyoyafanya kwenye mchezo uliopita wamejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho.

“Tunatarajia mchezo mzuri na wa ushindani tumejiandaa kushindana lolote linaweza kutokea Yanga ni timu kubwa inawachezaji wengi wazuri lakini tunahofia zaidi mchezaji aliyevaa jezi namba 9 (Mayele) na namba 6 (Fei Toto),” alisema na kuongeza.

“Tumekuja kupambana tutapambana hadi dakika ya mwisho bado tuna nafasi ya kufanya kitu  dakika 90 ndio zitaamua nani anatakiwa kuendelea hatua inayofuata,”

KUELEKEA MECHI YA CAF JUMAPILI…MGUNDA AWAANDALIWA WAMALAWI PIRA LA KITANGA….WAKIGUSA WANANATA WENYEWE…. KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO….UNAAMBIWA NABI HUKO YANGA HATAKI MZAHA…APANIA KUUA ‘SISIMIZI KWA RUNGU’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply