Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA CAF JUMAPILI…MGUNDA AWAANDALIWA WAMALAWI PIRA LA KITANGA….WAKIGUSA WANANATA WENYEWE….

admin September 16, 2022 4:10 pm


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba, amesema kuwa wanatambua mchezo wao ujao dhidi ya Big Bullets utakuwa mgumu hivyo wanajipanga kupata matokeo.

Mgunda ana kibarua cha kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo ujao wa kimataifa ambao ni wa awali baada ya ule wa kwanza kushinda.

 Mchezo huo dhidi ya Big Bullets unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 18, saa 1:00 usiku.

Katika mchezo wa awali uliochezwa, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 hivyo wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na faida ya mabao mawili.

Mgunda amesema:”Kumaliza kazi ya kwanza inatupa hatua nyingine kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa pili ambao utakuwa mgumu.

“Wachezaji wapo tayari na wanatambua kuwa mchezo utakuwa mgumu, ambacho tunakifanya ni kufanyia kazi makosa ambayo tuliyaona kwenye mchezo uliopita,” .

Ni mabao ya John Bocco na Moses Phiri yaliwapa ushindi Simba wakiwa ugenini kimataifa.

JICHO LA MGALILAYA : HILI LA TUISILA KISINDA LINA HARUFU YA RUSHWA….NINI KIMEWALAINISHA TFF ..? SAA CHACHE KABLA YA KUKUTANA NA YANGA KESHO….WASUDAN WAENDELEA KUWEWESEKA NA MAYELE…FEI TOTO KUTIWA PINGU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply