Home Yanga SC MUKOKO WA YANGA ANASAKWA NA VIGOGO AFRIKA

MUKOKO WA YANGA ANASAKWA NA VIGOGO AFRIKA


UONGOZI wa kikosi cha klabu ya Yanga umekiri kuwa Mkata umeme wao Mkongomani, Mukoko Tonombe anazivutia klabu nyingi kubwa barani Afrika, ambazo zimeonekana kuhitaji huduma ya mchezaji huyo.

Mukoko ambaye amebakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake na klabu ya Yanga ameonekana kuzivutia baadhi ya klabu kubwa wakiwemo wababe wa soka kutokea nchini Guinea, Horoya ambao wanatajwa kuweka dau la zaidi ya Shilingi Milioni 400 za Kitanzania kwa ajili ya kupata huduma yake.

Mukoko akiwa katika msimu wake wa kwanza tu ndani ya kikosi cha klabu ya Yanga, amefanikiwa kuhusika katika mabao nane akifunga mabao manne na kuasisti mabao manne mpaka sasa.

Akizungumzia ishu ya dili la Mukoko, Mkurugenzi wa mashindano wa klabu ya Yanga, Thabit Kandoro amesema: “Ni kweli zimekuwepo baadhi ya timu kubwa barani Afrika, ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji saini ya kiungo mkabaji wetu Mukoko Tonombe.

“Hii inatokana na ukweli kuwa kiungo huyo amekuwa katika kiwango bora msimu huu.”

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA RASMI KITAKACHOANZA DHIDI YA SIMBA