Home Simba SC SIMBA SC ‘YAFA KIUME’ LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA SC ‘YAFA KIUME’ LIGI YA MABINGWA AFRIKA


SIMBA imeaga rasmi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) kibabe, baada ya hatua ya robo fainali kuichapa Kaizer Chiefs mabao 3-0 mechi ya marudiano, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ilikuwa mechi ngumu kwao, kupambana na mlima mrefu wa mabao 4-0 waliofungwa nchini Afrika Kusini na Kaizer Chiefs.

Nahodha wa Simba, John Bocco alionyesha thamani ya kukabidhiwa beji hiyo na benchi la ufundi la timu yake, katika mechi hiyo,amepambana kwa kila hali kuipa timu yake ushindi, ingawa haujasaidia chochote zaidi ya kuweka heshima ya kutokufungwa nyumbani.

Bocco ameifungia Simba mabao mawili dakika ya 24 na 66, bao la pili amepokea pasi ya Luis Miqquissone, huku akikosa bao la tatu baada ya kuipaisha mpira juu dakika ya 68, akiwa amebaki yeye na kipa.

Simba imepata bao la tatu dakika ya 85 baada ya Chama kuwasoma mabeki wa Kaizer Chiefs kisha akapiga mpira pembeni na kuzitikisa nyavu zao.

Bao hilo liliwapa matumaini makubwa mashabiki wao kuamini kwamba wana uwezo wa kupindua meza kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa baada kupoteza ugenini mabao 4-0 nchini Afrika Kusini.

Lakini kadri dakika zilivyokuwa zinasonga mashabiki wa Simba walizidi kupata presha na kupoteza imani ya timu yao kushinda mabao mabao manne.

Simba imepambana kupigania tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini imeshindikana baada ya kumaliza dakika 90 kwa kushinda mabao 3-0.

Kaizar Chiefs imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuishinda Simba mabao 4-3.

SOMA NA HII  SIMBA HAWAPOI MAWINDO YANAENDELEA SASA WAHAMIA HUKU