Home Simba SC TANZIA: CLATOUS CHAMA AFIWA NA MKE WAKE NCHINI ZAMBIA

TANZIA: CLATOUS CHAMA AFIWA NA MKE WAKE NCHINI ZAMBIA

 


Kiungo Mchezaji wa Simba SC na timu ya taifa ya Zambia, Clatous Chama , amefiwa na mke wak e Mercy Munuka Chama  leo nchini Zambia.

Chama ambaye hivi sasa hayupo Tanzania, ambapo leo timu yake inacheza na Namungo FC.

Taarifa kutoka Zambia zinasema kuwa , Mrs Chama alikuwa akiumwa mno wiki nne zilizopita , hali iliyopeleka kulazwa katika hospitali ya Taifa ya Zambia.

Kutokana na hali ya aliyekuwa mkewe kuwa mbaya, Chama aliomba ruhusa kwa klabu yake na kwenda Zambia juzi, ambapo leo taarifa ya kifo cha mke wake imetoka.

Klabu ya Lusaka Dynamo ya Zambia, imetoa salamu za pole kwa Chama, ambapo awali  Chama aliichezea klabu hio.

Chama na Mercy Munuka wamejaliwa kuwa na watoto, ambapo anayefahamika na mashabiki wengi wa soka nchini ni mtoto wake wa kiume.


Aidha, katika miaka ya hivi karibuni, Mercy alikuwa akija Tanzania kushuhudia mechi mbalimbali ambazo mmewake alikuwa akicheza katika timu yake ya Simba SC.

Kama ilivyo tamaduni za kitanzania, Chama ambaye ni muumini wa dini ya kikristo, inatarajiwa taratibu zote za mazishi kufanana kama ambazo waumini wa dini ya kikristo hapa nchini huwa wanafanya.

Pamoja na kuwa haijawa rasmi, huenda Chama akaukosa mchezo wa watani wa jadi Simba vs Yanga unaotaraji kupigwa wiki ijayo jijini Dar es salaam.


Hii ni huenda ikasabishwa na yeye kuwa nchini Zambia kwa mapumziko mafupi mara baada ya kumzika mkewe siku chache zijazo.

Kikawaida, wakristo huchukua mpaka siku nne mpaka wiki kufanya ibada ya mazishi, kabla ya kufanya vikao vya familia na kuhitimisha tukio la msiba kwa mfiwa kupumzika kwa siku ama wiki kadhaa kabla ya kurudi kwenye majukumu yake ya kawaida.

Kwa kuzingatia uzito wa msiba huu, Soka la Bongo, tunatoa pole za dhati kwa wafiwa na wote walioguswa na msiba huu.

Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

SOMA NA HII  BAADA YA ISHU YA CHAMA KUPOA...MBRAZILI SIMBA AMUANZISHIA MTITI OKRAH...AMCHANA 'LIVE'...

1 COMMENT