Home Simba SC WATATU WA SIMBA HATIHATI KUIKOSA DODOMA JIJI KESHO

WATATU WA SIMBA HATIHATI KUIKOSA DODOMA JIJI KESHO


NYOTA watatu wa Simba, ambao ni Joash Onyango, Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin kuna hatihati wakaikosa Dodoma Jiji kesho katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 ambapo ni hatua ya robo fainali.

Mshindi wa mchezo wa kesho atakutana na mshindi wa mchezo wa Mei 26 kati ya Rhino Rangers na Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Nyota hao watatu walipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs.

Lwanga na Onyango hawa waligongana katika harakati za kuokoa hatari huku Mzamiru yeye alishindwa kumaliza mchezo huo kutokana na maumivu aliyopata. 

Kuhusu wachezaji ambao watakosekana kesho, Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba, amesema kuwa mazoezi ya leo jioni yatatoa muelekeo wa nani atakosekana na nani atakuwepo.

SOMA NA HII  KWA SIMBA HII, TATIZO NI MZAMIRU, ISHU IKO HIVI