Home Yanga SC YANGA YAENDELEA KUNG’ANG’ANIA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

YANGA YAENDELEA KUNG’ANG’ANIA UBINGWA WA LIGI KUU BARA


RAZACK Siwa, Kocha wa Makipa wa Klabu ya Yanga amesema kuwa bado wanang’ang’ania ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa bado hawajakata tamaa.

Ushindani wa kusaka taji la ligi ambalo lipo mikononi mwa Simba umezidi kushika kasi kwa timu zilizo ndani ya tatu bora ambazo ni Azam FC, Yanga pamoja na mabingwa watetezi Simba.

Baada ya ubao wa Jamhuri, Dodoma, jana Mei 19 kusoma JKT Tanzania 0-2 Yanga kumeifanya timu hiyo kufikisha alama 61 ikiwa nafasi ya pili na imecheza mechi 29 huku nafasi ya tatu ikiwa mikononi mwa Azam FC yenye pointi 57  na namba moja ni Simba ina pointi 61 na imecheza mechi 25.

Siwa amesema:”Tunashukuru Mungu kwa kucheza vizuri na kupata pointi tatu hilo ni jambo la msingi kwetu na kila mmoja.

“Kila kitu ni plan, (mpango) na tunapaswa tusiwe na haraka, tumeanza kufanya vizuri wakati huu na kupata pointi tatu, bado tunang’ang’ania ubingwa na tunapambana.

“Hatuwezi kuangalia nani ni nani jambo la msingi kwetu ni kushinda mechi zote ambazo zimebaki na hilo linawezekana,”.

Yanga imebakiwa na mechi tano kukamilisha msimu wa 2020/21 ikiwa imeshinda jumla ya mechi 17 ina sare 10 na imepoteza jumla ya mechi mbili sawa na Simba iliyo nafasi ya kwanza.



SOMA NA HII  PHIRI AFUNGUKA HAYA KUHUSU PENALTI ALIYOKOSA KWENYE NGAO YA JAMII