Home epl PEPE ATUPIA MAWILI ARSENAL IKIWAMALIZA CRYSTAL PALACE

PEPE ATUPIA MAWILI ARSENAL IKIWAMALIZA CRYSTAL PALACE


MIKEL Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal ameshuhudia vijana wake wakisepa na pointi tatu muhimu ugenini huku mchezaji wake Nicolas Pepe akirudi kambani mara mbili.

Ubao wa Uwanja wa Selhurst Park baada ya dakika 90 kukamilika usiku wa kuamkia leo ulisoma Crystal Palace 1-3 Arsenal. 

Pepe wa Arsenal alianza kupachika bao la kwanza dakika ya 35 ambalo liliwekwa sawa na Christian Bemtenke dakika ya 62.

Ni Gabriel Martinelli dakika ya 90+1 aliongeza bao kwa Arsenal na Pepe alikomelea msumari wa mwisho dakika ya 90+5.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya pointi 58 ikiwa nafasi ya 9 na Crystal Palace inabaki na pointi 44 ikiwa nafasi ya 13.


SOMA NA HII  WABAGUZI WAMSHAMBULIA NYOTA MANCHESTER UNITED