Home Ligi Kuu MWADUI FC SASA KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU UJAO

MWADUI FC SASA KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU UJAO


 KLABU ya Mwadui FC inayonolewa na Kocha Mkuu Salhina Mjengwa imekuwa ni timu ya kwanza kushuka daraja kwa msimu wa 2020/21 ndani ya igi Kuu Bara.

Kupoteza mbele ya Tanzania Prisons Mei 18, Uwanja wa Mwadui Complex kumeifanya timu hiyo kubaki na alama zake 19 ambazo hata ikishinda mechi zake nne zilizobaki haiwezi kutoka katika nafasi hiyo. 

Bao pekee la Mohamed Mkopi dakika ya 82 limeifanya timu hiyo kushuka daraja jumlajumla hivyo mechi zake za mwisho ni kukamilisha ratiba.

Zinabaki timu tatu kusaka nafasi ya kushuka daraja ili msimu ujao wa 2021/22 kuweza kushiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mwadui haikuanza msimu wa 2020/21 vizuri kwa kuwa ilianza kuyumba tangu kwenye mchezo wake wa awali na jambo hilo lilifanya kocha wao mkuu Khalid Adam kufutwa kazi.

Hata Amri Said naye alishindwa kuendelea na timu na badala yake alibwaga manyanga kutokana na kueleza kuwa hali ya ukata ilikuwa kubwa.

Ikiwa itaweza kushinda mechi zake zote nne ambazo zimebaki itavuna pointi 12 ambazo zitamfanya awe na pointi 31 ambazo Ihefu FC iliyo nafasi ya 19 na Gwambina FC iliyo nafasi ya 16 wanazo hizo pointi.

SOMA NA HII  MPAPATUKO WA NBC LIGI MZUNGUKO WA 18 UKO HIVI...FIFA YAIPA SIMBA KIPORO..YANGA KUKAMUANA NA HAWA...