Home Ligi Kuu HASARA YA VIPAJI IANDALIWE MAZINGIRA KUOKOLEWA

HASARA YA VIPAJI IANDALIWE MAZINGIRA KUOKOLEWA


KASI inazidi kuendelea kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa ushindani unazidi kuongeka na kila timu ikihitaji kupata kile inachohitaji yaani matokeo mazuri baada ya dakika 90.

Mwadui FC tayari wana tiketi mkononi ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza hivyo tayari kuna orodha ya wachezaji 30 ambao hawataonekana wakati ujao ndani ya Ligi Kuu Bara.

Hii ni hasara ya kwanza ambayo tumeshaanza kuiona hasa kwenye suala la vipaji ambavyo vilikuwa vinaonekana na kuna hatihati kati ya hao 30 ambao wapo ndani ya Mwadui FC wachache wanaweza kubaki ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.


Wapo wale ambao wanaweza kubaki kwenye ligi lakini ni mpaka pale watakapopata timu na wengine ni wale ambao wataamua kujiweka kando kwenye masuala ya soka katika hili ni muhimu kujiandaa vema kulinda vipaji hivi visipotee bure.


Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) liliweka wazi tangu awali mpango wa kupunguza timu kutoka 18 mpaka 16 ambapo zile zitakazokuwa nafasi ya 13 na 14 zitacheza playoff.

Kwa zile ambazo zitashuka zina jukumu la kujipanga upya na kufanya kazi kwa umakini katika kutimiza majukumu yao kwa sababu huku juu ushindani ni mkubwa muda wote.

Ukweli ni kwamba zile nne ambazo zitashuka maana yake ni kwamba zitashuka na wachezaji wake ambapo kwa nne ukitazaa kila timu kuwa na wachezaji zaidi ya 30 ni hasara kubwa ambayo tutaipata.


Katika hili nina amini kwamba TFF inaona wazi kwamba kuna umuhimu wa kuwalinda hawa vijana ili wasipotee kwenye ulimwengu wa mpira kwani wanahitajika na uwezo wanao ila mazingira yamewakataa kwa sasa.


Ikiwa watapewa nafasi ya kufanya vizuri huko wanakokowenda ni muhimu kutazama na kuwalinda ili waendelee kubaki katika ulimwengu wa mpira kwani vipaji wanavyo na wanaweza kufanya vizuri wakipewa nafasi.


Jambo la msingi ni kuweza kuandaa mazingira kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa kuweka ushindani kuwa mkubwa na kila timu kufanya vizuri huko kwenye mashindano ambayo wanashiriki.

SOMA NA HII  UBABEUBABE NDANI YA UWANJA UWEKWE KANDO, MPIRA BURUDANI

Ukweli ni kwamba kila mmoja ambaye anashuka daraja hapendi ila kwa kuwa mazingira yametokea na ni lazima iwe hivyo hakuna namna kinachotakiwa ni kuwalinda vijana waendelee kupambania ndoto zao.


Kwa wakati huu timu ambazo zipo kwenye lala salama basi zina kazi ya kuanza kujipanga upya angalau kupata kitu katika mechi hizi kwani maumivu hayaepukiki kwa namna yoyote ile.

Uzuri ni kwamba kabla ya msimu huu kuanza tuliongea kuhusu mipango ili kuona kwamba namna gani timu inaweza kupata matokeo chanya.


 Kwa kilichotokea mwanzo kwa wakati huu hakuna namna ya kubadili zaidi ya kuona kwamba kila mmoja anavuna kile ambacho anakipata uwanjani ila lazima apambane ili ashinde.


Suala la kushuka haliepukiki kwa namna yoyote ile jambo la msingi ni kujipanga vema ili kuweza kuwa imara kwa zile ambazo bado zina nafasi ya kupata matokeo.


Inawekezana zipo timu ambazo zipo mahali hapo kwa sasa kutokana na kushindwa kupata matokeo mazuri awali hivyo kama wakipata nafasi msimu ujao watakuwa na kazi ya kujipanga.


Kazi kubwa itakuwa kurekebisha yale makosa ambayo waliyafanya wakashindwa kufikia malengo ambayo walikuwa wamejipangia awali.


Wachezaji ambao walishindwa kuonyesha uwezo wao ni muda wao wa kupata changamoto mpya katika sehemu ambayo inawastahili tofauti na maisha ambayo waliishi wakati uliopita.


Kwenye maisha ya soka kila kitu kinawezekana na mambo kubadilika ni mara moja tu hivyo ikiwa walipata nafasi wakashindwa kuzitumia bado wana nafasi nyingine ya kuonyesha huko ambako watakwenda.

Wapo ambao watakwenda kwenye baadhi ya timu kwa mkopo na wapo ambao watakwenda katika timu zingine kupata changamoto mpya.

Kwa wale ambao watapata nafasi ya kucheza ndani ya dakika 90 basi wapambane kuipa timu matokeo ili kuona namna gani wanatimiza malengo yao kwa wakati.