Home Yanga SC BUMBULI: TUNA MECHI NNE ZIMEBAKI, TUTAPAMBANA KUFANYA VIZURI

BUMBULI: TUNA MECHI NNE ZIMEBAKI, TUTAPAMBANA KUFANYA VIZURI


  UONGOZI  wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kwenye mechi zao ambazo zimebaki ili kukamilisha ratiba kwa msimu wa 2020/21 na kupata kile ambacho wanakitarajia.

Yanga iliweka wazi kwamba inahitaji kutwaa taji la Kobe la Shirikisho pamoja na ligi. Na mataji yote hayo mawili mabingwa watetezu ni Simba.

Ikiwa itashinda mbele ya Biashara United kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho wa nusu fainali inaweza kukutana na Simba ama Azam FC ambazo zitakutana nazo kwenye mchezo wa nusu fainali.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara imecheza jumla ya mechi 29 imebakiwa na mechi tano ambazo ni dhidi ya Ruvu Shooting, Juni 17, Mwadui FC, Juni 20, Simba, Julai 3, Ihefu Julai 14 na kigongo cha mwisho ni dhidi ya Dodoma Jiji, Julai 18.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa:”Michezo minne imebakia kwa sasa, ambapo ni ule wa tarehe  17, 20 pia Kombe la FA tarehe 24. Mingine ni dhidi ya Ihefu na Dodoma ila tutaiwekea mipango namna ya kurudi baada ya kumaliza kwenye chezo wa Kombe la Shirikisho,”.

Chanzo: Azam 





SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LIGI...HILI HAPA BALAA LA YANGA YA GAMONDI....JE MOTO BADO UPO..?