Simba SC

DILI LA MANULA KWENDA MAMELOD SUNDOWNS LABUMA KISA 4G

admin June 2, 2021 4:47 am


IMEELEZWA kuwa kichapo cha mabao 4-0 ambacho Simba ilipata mbele ya Kaizer Chiefs kimebumisha dili la kipa namba moja Aishi Manula kusepa ndani ya timu hiyo.

Manula alikubali kuokota nyavuni mabao hayo wakati timu hiyo ilipokutana na Kaizer Chiefs nchini Afrika Kusini.

Habari zimeeleza kuwa timu ambayo ilikuwa inahitaji saini yake ambayo ni Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini iliamua kusitisha mpango huo.

Mtoa taarifa hiyo amesema kuwa mpango wa Mamelod Sundowns umesitishwa kwa kuwa kichapo kile kiliwashtua viongozi.

“Ikiwa amecheza mechi nyingi na alifanya vizuri basi alipaswa awe na mwendelezo pia katika mechi ya ushindani kwa kuwa ile ya Kaizer Chiefs alishindwa inaonyesha bado anahitaji muda,” .

ISHU YA METACHA MNATA KUSAJILIWA SIMBA IPO HIVI BEKI SILVA AANDALIWA MKATABA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply