ZIKIWA zimesalia mechi tano kwa upande wa Klabu ya Yanga ili kumaliza Ligi Kuu Bara msimu huu, uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi kuwa bado una matumaini ya kutwaa ubingwa.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 61, Simba ni kinara ana pointi 67.
Yanga imecheza jumla ya mechi 29 ndani ya ligi wakati Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 27.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa mechi ambazo zimebaki watapambana kupata matokeo chanya ili kufikia malengo yao.
“Matumaini ya ubingwa bado yapo kwa kuwa tuna mechi 5 ambazo tukishinda zote tunafikisha alama 15 ambazo bado zinatuweka kwenye mbio za ubingwa.
“Kwa hiyo hatujakata tamaa na sasa hivi timu inaendelea kujiandaa kuelekea michezo ijayo,” amesema Bumbuli.
Juni 6 kikosi kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon, Uwanja wa Azam Complex.