Home Azam FC AWESU AWESU NYOTA ANAYEPAMBANA NA HALI YAKE NDANI YA AZAM FC

AWESU AWESU NYOTA ANAYEPAMBANA NA HALI YAKE NDANI YA AZAM FC


NYOTA Awesu Awesu moja ya viungo wazawa wazuri wenye uwezo ndani ya uwanja ila anakosa nafasi ndani ya Azam FC ya George Lwandamina kutokana na ushindani wa namba.


Nyota huyo aliibuka ndani ya Azam FC akitokea Klabu ya Kagera Sugar iliyokuwa inanolewa na Mecky Maxime ambaye alichimbishwa ndani ya kikosi hicho.


Alikuwa anatajwa pia kuingia anga za Yanga ila walipishana kidogo kwa upande wa maslahi na mabosi wa Yanga wakamvuta Zawadi Mauya.

Pia kwa sasa Mauya naye ndani ya Yanga mambo ni magumu kutokana na kushindwa kufurukuta kikosi cha kwanza.

Msimu wa 2019/20 Awesu aliweza kutupia jumla ya mabao 7 katika mashindano yote ambayo alishiriki ikiwa ni Ligi Kuu Bara alitupia mabao 6 na ndani ya Kombe la Shirikisho alitupia bao moja.

Bao hilo moja aliwatungua Yanga ilikuwa ni kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa na hakumaliza dakika 90 kwa kuwa alionyeshwa kadi nyekundu.

Habari zinaeleza kuwa huenda atatolewa kwa mkopo msimu ujao ili akapate changamoto mpya kwa kuwa kwa sasa anapambana na hali yake ili aweze kuwa bora.

SOMA NA HII  JESHI LA AZAM FC LATUA KWA KIBABE MISRI....WAARABU WATETEMEKA