MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Bongo, Oscar Oscar ameweka wazi kwamba ana nia ya kuwania Uraisi wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) na anaamini kwamba anatosha katika eneo hilo huku akiamini kwamba ni ngumu kubadili mpira ikiwa hautakuwa ndani ya maamuzi. Malengo yake ni kuongoza mpira katika hatua ya juu ikiwa ni pamoja na FIFA.