Yanga SC

YANGA YASHUSHA PRESHA ISHU YA MUKOKO TONOMBE

admin June 9, 2021 5:47 am


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hali ya kiungo wao Tonombe Mukoko, ambaye alipata majeruhi akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa kwa sasa inaendelea vizuri.


Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa walipata taarifa kuhusu kuumia kwa mchezaji wao.

Bumbuli amesema:-“Tulikuwa na wasiwasi juu ya hali ya mchezaji Mukoko Tonombe ambaye aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Tunisia.

“Ila kwa sasa tumepata taarifa kwamba anaendelea vizuri na tumewasiliana naye kama klabu na hatua inyofuata ni madaktari kuzungumza na madaktari wa huko ili kujua kwamba kama anaweza kukaa nje kwa muda gani,” amesema Bumbuli.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO VIDEO: MAZOEZI YA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA KUELEKEA KWENYE MCHEZO DHIDI YA MALAWI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply